Kwanini Kujiondoa kwa Marekani NATO ni hatari kwa Muungano huo? - Fastestsmm News Swahili

0
Kwanini Kujiondoa kwa Marekani NATO ni hatari kwa Muungano huo? - Fastestsmm News Swahili

Chanzo cha picha, EPA

Gazeti la The Guardian la Uingereza lilitoa maoni yake katika tahariri yake kuhusu mkutano wa kilele wa Jumuiya ya Kujihami ya NATO, uliomalizika nchini Lithuania siku ya Jumatano, na changamoto kubwa zinazosubiri nchi za NATO.

Miongoni mwa changamoto kubwa zinazotishia muungano huo ni uwezekano wa Marekani kujitoa katika muungano huo, hasa iwapo Donald Trump atarejea tena Ikulu ya White House, jambo ambalo litaiacha Ulaya katika mzozo wa kiusalama na kijeshi.

Gazeti hilo lilisema kwamba hakukuwa na uwezekano wa kutokea mshangao katika mkutano huu, haswa kuhusiana na kujitosa kwa Ukraine, ambayo isingeweza kujiunga nayo wakati ipo katika hali ya vita, na uanachama inaoutaka usingeweza kutolewa tena katikati ya mzozo huo.

Kifungu cha 5 cha muungano huo, ambacho kinafafanua kanuni ya ulinzi wa pamoja - shambulio kwa mwanachama yeyote linachukuliwa kama shambulio kwa wote, linakusudiwa kuzuia vita, na sio kupigana vita.

[ad_2] #Kwanini #Kujiondoa #kwa #Marekani #NATO #hatari #kwa #Muungano #huo #Fastestsmm #News #Swahili

Post a Comment

0Comments
Post a Comment (0)
To Top