Wanachama wa Nato wanafikiria kutuma silaha zaidi na risasi kwa Ukraine ili kuisaidia kujilinda dhidi ya uvamizi wa Urusi. Marekani ndiyo mchangiaji mkubwa wa misaada ya kijeshi - kwa mbali ikifuatiwa na Umoja wa Ulaya (EU), Ujerumani na Uingereza.
Kiasi cha usaidizi wa kijeshi unaotolewa kwa Ukraine hufuatiliwa na Taasisi ya Keil. Na Marekani imetangaza msaada mpya wa kijeshi kwa Ukraine wenye thamani ya dola milioni 500.
Marekani pia imethibitisha kuwa itatoa silaha za cluster, uamuzi ambao umeleta utata na kusababisha wasiwasi miongoni mwawashirika wa Nato. Ukraine pia itapokea makombora kutoka Ufaransa - sawa na makombora ya Uingereza Storm Shadows ambayo yalitolewa hivi karibuni.
Vifaru
Kuna ahadi ya kutolewa dazeni ya vifaru. Ukraine inasema inahitaji kulinda eneo lake na kuwaondoa wanajeshi wa Urusi.
• Marekani inatuma vifaru vyake 31 vya Abrams
• Uingereza inatoa vifaru 14 ya Challenger 2
• Ujerumani inatoa vifaru 14 ya Leopard 2
• Uhispania inasema itatuma vifaru sita vya Leopard 2.
Vifaru vya Leopard 2 hutumiwa na nchi nyingi za Ulaya, na vinaelezwa ni rahisi kuvitunza na havitumii mafuta mengi kama vifaru vingine.
Katika miezi ya kwanza baada ya uvamizi huo, Nato ilipendekeza nchi wanachama kusambaza Ukraine vifaru vikongwe. Wanajeshi wa Ukraine wanajua jinsi ya kuviendesha, na jinsi ya kuvitunza, na walikuwa na vipuri vya kutosha.
Vifaru vingi vya kisasa vya Magharibi ni vigumu kuvitumia na kuvitunza. Picha za hivi karibuni za shambulio la Ukraine kwenye himaya za Urusi zinaonyesha vifaru vya Leopard na Bradley tayari vinatumiwa na vikosi vya Ukraine.
Uingereza ilikuwa ya kwanza katika Nato kutoa kifaru cha Challenger 2. Challenger 2 kiliundwa miaka ya 1990. Ndio kifaru bora zaidi miongoni wa vifaru vinavyotumiwa na vikosi vya Ukraine. Tangu Februari 2022 imepokea zaidi ya vifaru 200 aina ya T-72s, kutoka Poland, Jamhuri ya Czech na nchi nyingine.
Akitangaza uamuzi wa Marekani wa kutuma vifaru 31 vya Abrams nchini Ukraine, Rais Joe Biden alivitaja kuwa "vifaru vyenye uwezo mkubwa zaidi duniani." Alisema Marekani itaanza kuwafunza wanajeshi wa Ukraine kuvitumia lakini bado haijafahamika itachukua muda gani hadi vifaru vyenyewe kuwasili.
Wanajeshi wa Ukraine wanatarajiwa kumaliza mafunzo ya vifaru vya Abrams ifikapo mwisho wa majira ya joto, kulingana na ripoti kutoka vyombo vya habari vya Marekani.
Magari ya vita
Wataalamu wa kijeshi wanaeleza kwamba mafanikio kwenye uwanja wa vita yanahitaji silaha nyingi. Stryker ni mojawapo ya magari ya kivita ambayo yametolewa kwa Ukraine. Marekani ilithibitisha kuwa Strykers 90 yatatumwa.
Miongoni mwa magari mengine yaliyotolewa na Marekani ni magari ya Bradley. Ambayo yalitumiwa sana na majeshi ya Marekani nchini Iraq.
Ulinzi wa anga
Mwezi Disemba, Marekani pia ilitangaza kutuma mfumo wa makombora wa Patriot nchini Ukraine - na Ujerumani na Uholanzi zimefuata mkondo huo.
Mfumo huu wa hali ya juu husafirisha kombora hadi kilomita 100km, kulingana na aina ya kombora linalotumika, na unahitaji mafunzo maalum kwa wanajeshi wa Ukraine, ambayo huenda yakafanyika katika kambi ya Jeshi la Merikani huko Ujerumani.
Lakini mfumo huo ni ghali kuuendesha - kombora moja la Patriot linagharimu takriban dola milioni 3m. Tangu kuanza kwa vita, Ukraine imekuwa ikitumia mifumo wa ulinzi wa wa S-300 ambao ni wa tangu enzi za Usovieti ya dhidi ya mashambulizi ya Urusi.
Marekani pia imetoa Nasams, mfumo wa ulinzi wa anga kwa Ukraine. Mfumo huo ulifika Ukraine mnamo Novemba. Kwa kuongeza, Uingereza imetoa mifumo kadhaa ya ulinzi wa anga, ikiwa ni pamoja na Starstreak, iliyoundwa kuangusha ndege zinazoruka chini za masafa mafupi.
Ujerumani pia imetoa mifumo ya ulinzi wa anga, ikiwa ni pamoja na mifumo ya ulinzi ya anga ya IRIS-T ambayo inaweza kupiga makombora kwa umbali wa hadi kilomita 20.
Miongoni mwa makombora ya masafa marefu yaliyotumwa Ukraine na Marekani ni yale ya Himars. Nchi kadhaa za Ulaya pia zimetuma mifumo kama hiyo. Himars inaaminika kuwa kitovu cha mafanikio ya Ukraine katika kurudisha nyuma vikosi vya Urusi kusini, haswa huko Kherson mnamo Novemba. Himars inakwenda masafa marefu zaidi kuliko mfumo wa Smerch unaotumiwa na Urusi.
Silaha nyingine
Katika miezi iliyofuata baada ya uvamizi na Urusi kurudi nyuma kutoka Kyiv, vita vilihamia mashariki mwa nchi ambapo usambazaji wa silaha kwa Ukraine ulikuwa na umuhimu mkubwa.
Australia, Canada na Marekani zilikuwa miongoni mwa nchi zilizotuma mizinga ya hali ya juu aina ya M777 na risasi kwa Ukraine. Uwezo wa M777 ni sawa na mizinga ya Giatsint-B ya Urusi.
Nchi za Nato zinasema kuwa zinapanga kuongeza usambazaji wao wa makombora, kwa sababu Ukraine imekuwa ikiyatumia kwa wingi sana. Wamewataka wazalishaji wao wa ndani kuongeza uzalishaji.
Maelfu ya silaha za Nlaw, iliyoundwa kuharibu vifaru kwa pigo moja, pia zimetolewa kwa Ukraine. Silaha hizo zinafikiriwa kuwa muhimu sana katika kuzuia kusonga mbele kwa vikosi vya Urusi huko Kyiv baada ya uvamiz.
Ndege zisizo na rubani zimehusika sana katika mzozo huo hadi sasa, huku nyingi zikitumika kwa uchunguzi, ushambuliaji na shughuli za kunyanyua vitu vizito.
Uturuki imeuza ndege zisizo na rubani aina ya Bayraktar TB2 kwa Ukraine, huku kampuni ya Uturuki inayotengeneza mfumo huo imetoa msaada wa ndege zisizo na rubani kwa ajili ya kuunga mkono Ukraine.
Wachambuzi wanasema TB2 za Bayraktar zimekuwa na ufanisi mkubwa, zikiruka kwa takriban futi 25,000 (mita 7,600) kabla ya kushuka kushambulia maeneo ya Urusi kwa mabomu yanayoongozwa na mionzi.
Marekani ilikuwa imepinga ombi la Ukraine la kutaka ndege za kivita. Lakini mwezi Mei, Rais Joe Biden alitangaza Marekani itaunga mkono kutoa ndege za kivita - ikiwa ni pamoja na F-16 zilizotengenezwa Marekani - kwa Ukraine na pia kurejea kutoa mafunzo kwa marubani wa Ukraine kuziendesha.
Uidhinishaji huo wa Marekani utaruhusu mataifa mengine kuuza nje ndege zao za F-16, kwani Marekani inapaswa kuidhinisha kisheria uuzaji wa vifaa vilivyonunuliwa na washirika.
Uingereza, Uholanzi, Ubelgiji, Ufaransa na Denmark zimekaribisha hatua hiyo na zitatoa msaada.
Post a Comment
0Comments