Biden kukutana na Waziri mkuu wa Uingereza Sunak na Mfalme Charles kuhusu hofu ya mabomu ya Cluster Ukraine - Fastestsmm Swahili

Novah
By -
0
Biden kukutana na Waziri mkuu wa Uingereza Sunak na Mfalme Charles kuhusu hofu ya mabomu ya Cluster Ukraine - Fastestsmm Swahili

Copyright: Reuters

Rais wa Marekani Joe Biden amewasili nchini Uingereza kabla ya kufanyika mkutano wa kilele wa Nato nchini Lithuania baadaye wiki hii – unaojiri baada ya washirika kadhaa kuhoji wito wake wa kutuma mabomu ya kutawanyika nchini Ukraine Cluster bombs

Uingereza na Canada ni miongoni mwa wale waliotilia shaka upelekaji wa mabomu hayo , ambayo yamepigwa marufuku kutokana na hatari yanayosababisha kwa raia.

Marekani inasema kwamba mabomu hayo yanahitajika kwasababu hifadhi ya silaha ya Ukraine inapungua.

Siku ya Jumatatu , bwana Biden atakutaka na waziri mkuu wa Uingereza Rishi Sunak .

Wawili hao wanatarajiwa kujadiliana kuhusu masuala kadhaa , ikiwemo vita vya Ukraine.

Bwana Sunak hajamkosoa moja kwa moja mwenzake wa Marekani kufuatia tangazo la Ijumaa la mabomu hayo ya Cluster – lakini siku ya Jumamosi alisema kwamba Uingereza ni mojawapo ya mataifa 123 yaliotia Saini makubaliano kuhusu silaha za Cluster , makubaliano ya kimataifa ambayo yanapiga marufuku uzalishaji ama matumizi ya silaha hizo.

Lakini washirika wengine wa Marekani wameongezea. Mshirika wa Nato New Zealandalisema siku ya Jumapili silaha hizo zinaweza kusababisha madhara mabkubwa kwa raia wasio na hatia.

Mabomu ya kutawanyika kwa kawaida hutoa mabomu mengi madogo ambayo yanayoweza kuua kiholela katika eneo kubwa. Mabomu ambayo hayajalipuka yanaweza kukaa ardhini kwa miaka kadhaa kabla ya kulipuka.

Marekani inasema imepokea uhakikisho wa maandishi kutoka kwa Kyiv kwamba wanajeshi wa Ukraine hawatatumia silaha hizo nchini Urusi au katika maeneo ya mijini.

Akiwa nchini Uingereza, Bw Biden pia atakutana na Mfalme Charles kwa mara ya kwanza tangu Mfalme kutawazwa.

Wanachama wa Nato - muungano wa kijeshi wa mataifa 31 ya Magharibi - kisha watakutana Vilnius siku ya Jumanne na Jumatano kuongeza akiba ya risasi na kukagua mipango ya ulinzi itakayokuwa kwenye ajenda.

Finland itahudhuria mkutano wake wa kwanza tangu ijiunge na Nato mwezi Aprili, na mipango kutoka Uswidi kufuata mkondo huo imezuiwa na Uturuki, ambayo inaishutumu kwa kuwahifadhi magaidi. Bw Biden anatarajiwa kutafuta uungwaji mkono kutoka kwa Bw Sunak ili kusaidia kufanya makubaliano na Uturuki.

Ukraine ina matamanio yake ya kujiunga na Nato. Lakini akizungumza na CNN kabla ya safari yake, Bw Biden alisema hilo haliwezi kutokea hadi vita viishe - kulingana na sera ya muda mrefu ya muungano huo.

Akitoa mfano wa mkataba wa ulinzi wa pande zote wa Nato, Bw Biden alisema kuwa wanachama wanajitolea kulinda "kila inchi" ya eneo la kila mmoja - akimaanisha kwamba "ikiwa vita vinaendelea, basi sote tuko vitani".

Rais wa Ukraine Volodymyr Zelensky amekubali msimamo huu hapo awali, huku akiomba "ishara" kwamba nchi yake itaweza kujiunga na muungano huo vita vitakapomalizika. Anatarajiwa kuhudhuria mkutano wa kilele wa wiki hii.

[ad_2] #Biden #kukutana #Waziri #mkuu #Uingereza #Sunak #Mfalme #Charles #kuhusu #hofu #mabomu #Cluster #Ukraine #Fastestsmm #Swahili

Post a Comment

0Comments

Post a Comment (0)