Maandamano Kenya:Mateso yatakuwa jambo la kawaida iwapo Ruto ataruhusiwa kutekeleza Sheria ya Fedha-Raila - Fastestsmm News Swahili

Novah
By -
0
Maandamano Kenya:Mateso yatakuwa jambo la kawaida iwapo Ruto ataruhusiwa kutekeleza Sheria ya Fedha-Raila - Fastestsmm News Swahili

Chanzo cha picha, AFP

Kiongozi wa upinzani nchini Kenya amesema Wakenya wataendelea kuteseka iwapo serikali yar ais William Ruto itaruhusiwa kutekeleza sheria ya fedha inayopendekeza kuongezwa kwa ushuru .

Katika mkutano na waandishi wa habari ,Odinga ametangaza kuahirisha mkutano wa hadhara katika eneo la Kamukunji jijini Nairobi kutokana na kile alichosema ni ‘njama ya kuwashambulia viongozi wa Azimio’.

Amesema hali ya kawaida itarejelewa tu wakati rais Ruto atakapojitokeza na kubadilisha sheria hiyo na kutangaza mikakati ya kupunguza gharama ya maisha Pamoja na kukubali mazungumzo ya kuunda upya tume ya uchaguzi na mipaka .

Maelezo ya video,

Jinsi polisi walivyokabiliana na waandamanaji nchini Kenya

Odinga amesema maandamano yanayoongozwa na upinzani ni ya amani na ghasia hutokea wakati polisi wanapoingilia kuyavunja na kuwatupia vitoa machozi waandamanaji .

[ad_2] #Maandamano #KenyaMateso #yatakuwa #jambo #kawaida #iwapo #Ruto #ataruhusiwa #kutekeleza #Sheria #FedhaRaila #Fastestsmm #News #Swahili

Post a Comment

0Comments

Post a Comment (0)